Katika ujumbe wa Twitter, wizara hiyo imesema kwamba wanajeshi wa Russia wamefanya kazi kuimarisha kikosi chao kwa kutarajia mashambulizi makali kutoka kwa Ukraine katika sehemu za kaskazini mwa Luhansk au Zaporizhzhia.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba endapo wanajeshi wa Ukraine watafanikiwa kuiteka Zaporizhzhia, watakuwa wamepiga hatua kubwa sana na kudhoofisha uwezo wa Russia kutumia daraja linalounganisha mkoa wa Rostov nchini Russia na Crimea.
Imeongezea kusema kwamba mafanikio ya wanajeshi wa Ukraine katika mkoa waLuhansk yatapelekea malengo ya Russia ya kutwaa Donbas kufifia kwa kiwango kikubwa.
Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kwamba Russia haijafanya uamuzi kuhusu sehemu ambayo wanastahili kuweka nguzu zao nyingi na maafisa wa kufanya mikakati na maamuzi wanakabiliwa na wakati mgumu kuchukua uamuzi wa mwisho.
Mapigano yaliendeela Jumamosi katika mji wa Bakhmut, licha ya rais wa Russia Vladimir Putin kutangaza usitishwaji wa vita kwa muda wa saa 36 kwa ajili ya sherehe za krismasi kwa waumini wa dhehebu la Orthodox.