Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:55

Ukraine: Kombora la Russia lashambulia soko la mkoa wa Kharkiv


Kikosi cha zimamoto kikikabiliana na mlipuko wa kombora lililopigwa na Russia katika soko mjini Shevchenkove, Mkoa wa Kharkiv , Ukraine Jan. 9, 2023. (Governor of Kharkiv region Oleh Sunehubov via Telegram/Handout via Reuters)
Kikosi cha zimamoto kikikabiliana na mlipuko wa kombora lililopigwa na Russia katika soko mjini Shevchenkove, Mkoa wa Kharkiv , Ukraine Jan. 9, 2023. (Governor of Kharkiv region Oleh Sunehubov via Telegram/Handout via Reuters)

Maafisa wa Ukraine Jumatatu walisema kombora la Russia lilipiga soko moja katika mkoa wa Kharkiv, na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.

Maafisa walisema kombora hilo lilipiga katika kijiji cha Shevchenkove, kilichopo kilomita 75 kutoka mji wa Kharkiv.

“Tunalaani kitendo hiki cha kigaidi,” Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Emine Dzhaparova alituma ujumbe wa Twitter pamoja na picha ya video na picha nyingine zinazoonyesha shimo kubwa na jengo likiwaka moto. “Majibu pekee sahihi ni kwa Ukraine kupatiwa silaha zaidi.”

Russia imerejea mara kadhaa kuonya dhidi ya msaada wa kijeshi wa nchi za Magharibi kwa Ukraine, ikisema silaha zinazopelekwa kutoka Marekani na washirika wa Ukraine Ukraine utauzidisha mzozo.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari katika maelezo aliyoyatoa Jumatatu kwamba silaha zaidi zinazotolewa na nchi za Magharibi “zitachochea zaidi mateso wanayoyapata watu wa Ukraine.”

Russia ilianzisha uvamizi wa Ukraine takriban miezi 11 iliyopita, na kufanya kuwepo kura ya haraka ya walio wengi katika Baraza Kuu la UN wakilaani operesheni na kuitaka Russia iondoe majeshi yake.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya usiku Jumapili kuwa wiki ya kwanza ya mwaka mpya haijaleta mabadiliko muhimu katika mstari wa mbele wa vita hivi, badala yake kumekuwa na mapigano makali yakiendelea katika mikoa ya Luhansk na Donetsk mashariki mwa Ukraine,

Zelenskyy highlighted the fight for the city of Bakhmut, calling it “one of the bloodiest places on the frontline.”

Zelenskyy ameelezea mapigano katika mji wa Bakhmut, akiyaita “moja ya maeneo yenye umwagaji damu mkubwa katika mstari wa mbele wa vita.”

XS
SM
MD
LG