Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:19

Zelenskiy aomba Ukraine iondolewe udhibiti wa makombora ya masafa marefu


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alipofanya mkutano na vyombo vya habari Kyiv Agosti 27, 2024. Picha na REUTERS/Valentyn Ogirenko
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alipofanya mkutano na vyombo vya habari Kyiv Agosti 27, 2024. Picha na REUTERS/Valentyn Ogirenko

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema siku ya Jumatano kuwa shambulizi la anga la Russia mapema siku hiyo katika mji wa mashariki wa Kupyansk limesababisha vifo, bila ya kutoa idadi.

Zelenskiy pia amesema katika hotuba yake ya kila usiku kuwa Magharibi kuondoa masharti kwa mashambulizi ya anga ya masafa marefu yanayofanywa na Ukraine kwa sababu yataisaidia kumaliza vita.

“Pia tunafanyakazi na washirika kupata vifaa kwa ajili ya vita. Si tu silaha na risasi, lakini pia kuimarisha umoja wetu na washirika. Umoja wenye ufanisi - wa masafa marefu,” alisema.

“Tunaendelea kusisitiza kuvimaliza vita kwa haraka, kuondoa haraka masharti kwa matumizi ya makombora ya masafa marefu haraka kwa Ukraine, kutatusaidia kumaliza vita haraka iwezekanavyo kwa Ukraine na dunia nzima kwa ujumla” aliongeza

Forum

XS
SM
MD
LG