Kyiv imesema, mashambulizi hayo ambayo yalilenga mikoa 10, yanaonekana yalikuwa yamepangwa vizuri ili kuharibu mitambo ya umeme ya Ukraine kabla ya msimu wa baridi ambapo wananchi wake huitaji zaidi umeme na mifumo ya joto.
Shambulizi hilo lilikuwa shambulizi kubwa la Russia katika kipindi cha wiki kadhaa, siku 20 baada ya Ukraine kuishtukiza Moscow kwa kuvuka mpaka na kuingia katika mkoa wa Russia wa Kursk, ambako Ukraine iliua na kuwateka nyara wapiganaji wengi wa Russia.
Hata hivyo, wanajeshi wa Russia walisonga mbele mashariki mwa Ukraine, na kufunga kitovu cha usafiri cha Pokrovsk.
Kwenye mtandao wa Telgram, Rais wa Ukraine Voldymyr Zelenskiy amelitaja shambulizi la Jumatatu kuwa “moja ya mashambulizi makubwa. Zaidi ya makombora 100 ya aina mbalimbali na karibu ndege 100 zisizo na rubani.
Zelenskiy alisema miundombinu ya nishati iliharibiwa sana.
Forum