Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:47

Russia na Ukraine zaendelea na mashambulizi


Russia na Ukraine, Jumamosi zimejibizana katika mapambano ya ndege zisizo na rubani, makombora na silaha nyingine wakati Kyiv ikiadhimisha kwa mara ya tatu siku ya uhuru toka Moscow kuanza uvamizi kamili.

Mwanamke mmoja aliuwawa na mwanaume kujeruhiwa wakati vikosi vya Russia viliposhambulia mji wa kusini mwa Russia, Kherson, mji mkuu wa eneo lililovamiwa la Kherson kwa mujibu wa mwendesha mashitaka wa mkoa huo.

Kikosi cha anga cha Ukraine kimesema kilizuia na kuziharibu ndege zisizo na rubani saba zilizofika eneo la kusini mwa nchi.

Mabomu ya masafa ya mbali ya Russia, pia yalitumika kushambulia eneo la kisiwa cha Zmiinyi, huku eneo kubwa la mkoa wa Kherson likikabiliwa na mabomu kutoka angani.

Kwa upande wa Russia, wizara ya ulinzi, Jumamosi imeeleza kwamba kikosi cha ulinzi wa anga kilitungua ndege saba zisizo na rubani nyakati za usiku.

Forum

XS
SM
MD
LG