Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:30

WTO inamatumaini ya kufikia makubaliano ya biashara ya uvuvi


Mkurugenzi Mkuu Ngozi Okonjo-Iweala
Mkurugenzi Mkuu Ngozi Okonjo-Iweala

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani, WTO, amewaambia mawaziri wa biashara ana matumaini mazuri ya kufikia makubaliano juu ya mazungumzo ya biashara ya uvuvi duniani.

Lakini, wakati huohuo ametoa wito kwa mataifa kubadili fikra na mitazamo yao ili kuweza kusuluhisha tofauti zilizopo.

Mawaziri na wataalamu kwenye mkutano wa WTO, kupitia mtandaoni, uliofanyika kutoka Geneva Alhamisi, wana matumaini hatimaye kufikia makubaliano juu ya tatizo la uvuvi kupindukia mpaka baada ya kujaribu kwa miaka 20.

Mkutano wa WTO
Mkutano wa WTO

Akihutubia mkutano huo wa kwanza wa mawaziri wa biashara wa mataifa 164 wanachama wa WTO kufanyika tangu 2017, Mkurugenzi Mkuu Ngozi Okonjo-Iweala amesema ana amini kila mtu ana nia ya dhati kuona makubaliano yanafikiwa.

Mkurugenzi mkuu wa WTO ameeleza : "Waheshimiwa nina amini kwamba sote tuna dhamira ya dhati, lakini inahitajika tubadili fikira na mtizamo wetu ili tuweze kuunganisha mianya ya mwisho inayotutenganisha sisi wanachama. Nimeuitisha mkutano huu kwa sababu tunahitaji uongozi wetu wa pamoja wa kisiasa kuweza kusukuma majadiliano ya awamu ya mwisho ili tuweze kuwasilisha mkataba hivi karibuni."

Shirika hilo la Umoja wa Matiafa halijafanikiwa kufikia makubaliano ya kimataifa kwa miaka mingi na Okonjo-Iweala aliyechukua uongozi mwezi Machi mwaka 2021 anasema mazungumzo hayo yanabidi kuwa mtihani mkuu kwa shirika hilo juu ya uwezo wake wa kutekeleza mambo.

Okonjo-Iweala : "Ni miaka 20 tangu kuanza mazungmzo haya na bado hatujaweza kufikia makubaliano. Tabia ya uvuvi usio katika hali ya endelevu unaendelea kuathiri vibaya bahari zetu, na hivyo basi tuna tafuta msaada wa kifedha kutoka serikali zetu ili tukomeshe hali hii. Waheshimiwa wakati umefika wa kuchukua hatua thabiti."

Na katika ishara ya kutia moyo mteja mkuu wa uvuvi, Umoja wa ulaya amesema kwamba mswaada wa mkataba uliyopo unaweza kuwa msingi wa kufikia makubaliano ya kimataifa kwa vile una vipingele vingi vya kuridhisha kanda zote.

Hata hivyo kuna baadhi ya wajumbe wanaosema kwa faragha kwamba bado kuna tofauti katika suala la ruzuku zinaotolewa kati ya nchi Tajiri kama zile za Umoja wa Ulaya na nchi zinazoendelea kama India na nyenginezo.

Mwenyekiti wa majadiliano kuhusu ruzuku balozi wa Colombia kwenye WTO, Santiago Wills, anasema mazunguzmo yalianza 2001 na yamepitwa na wakati kutokana na maendeleo yanayotokea duniani na hivyo kuna haja ya kufikiwa makubaliano haraka.

Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala akiwa na Balozi wa Colombia katika WTO Santiago Wills
Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala akiwa na Balozi wa Colombia katika WTO Santiago Wills

Balozi wa Colombia kwenye WTO ameeleza : "Hii sio namna WTO hufanya kazi kuhusiana na ushirikiano wa kibiashara. Mazungumzo yalipoanza kulikuwa na dharura miaka 20 iliyopita na imezidi kuongezeka kila mwaka unapopita, na akiba ya samaki kuendelea kupunguka sana. Kwa hivyo muda wa kufikia makubaliano umefika na dunia inatutizama."

Mbali na tatizo hilo shirika hilo linakabiliana na mvutano juu ya namna ya kutanzua ugomvi na wachambuzi wanasema inabidi kwa WTO kufikia mkataba angalau moja mwaka huu kuweza kuendelea kuthaminiwa.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG