Karibu kesi 17,500 za ugonjwa wa surua zimerekodiwa katika eneo la Afrika kati ya mwezi Januari na Machi mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 400 ikilinganishwa na wakati kama huo mwaka 2021.
Nchi 20 za Afrika zimeripoti ugonjwa wa surua katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni nane zaidi kuliko hivyo katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka 2021.
Milipuko ya magonjwa mengine yanayoweza kuzuilika kwa chanjo yamekuwa ya kawaida.
Nchi 24 zimethibitisha mlipuko wa ugonjwa wa kupooza mwaka 2021, ambayo ni zaidi ya mara nne kuliko ilivyokuwa mwaka 2020.
Mwaka 2021, nchi 13 zimeripoti milipuko ya homa ya manjano katika eneo la Afrika, ikilinganishwa na mwaka 2020 na nyingine tatu mwaka 2019.