Taifa hilo la pili lenye uchumi mkubwa duniani limekuwa likisumbuka kudhibiti mlipuko wake mbaya katika miaka miwili, huku likiweka masharti makali kwa kufunga shughuli zote na kufanya upimaji wa watu wengi kwa kushikilia sera kali ya kutopatikana hata kisa kimoja cha maambukizi ya Covid, ikiathiri sana biashara na ari ya umma.
Mji ambao ni kitovu cha biashara wa Shangai umefungwa kabisa tangu mwanzoni mwa mwezi huu, na hivo kusababisha tatizo la usambazaji wa bidhaa, huku wakazi wengi wakizuiliwa majumbani mwao kwa muda mrefu zaidi kwa sababu umekuwa kitovu cha mlipuko wa Covid 19.