WHO imesema wanafuatilia kwa karibu kuhusu dalili zozote walizonazo na utoaji wa chanjo utaanza katika siku chache zijazo.
Mwishoni mwa wiki maafisa wa afya walitangaza mlipuko wa tatu wa Ebola katika jimbo la Equateur tangu mwaka 2018.
Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 31 aliyeambukizwa virusi hivyo kwenye mji wa Mbandaka alifariki.
DRC imekumbwa na milipuko 14 ambayo imesababisha vifo vya maelfu ya watu.