Watu wawili wanajulikana kuwa wamefariki hadi sasa katika mji huo wenye wakazi zaidi ya milioni moja ambako watu wanaishi karibu na barabara, maji na njia za anga kuelekea katika mji mkuu Kinshasa.
Kifo cha kwanza kilitokea April 21 na cha pili Jumanne ikiwa ni mlipuko wa 14 wa Ebola katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
Karibu dozi 200 za chanjo ya Ebola zimepelekwa mbandaka kutoka mashariki mwa Goma na nyingine zinatarajiwa kupelekwa katika siku zijazo, WHO imesema katika taarifa yake.
Majopo matatu ya wataalamu wa chanjo yapo huko na yatalenga zaidi kwa watu ambao wako hatarini kuambukizwa.