Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:47

WHO yasisitiza watu kujikinga na COVID-19 kwa kufuata masharti


 Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya Jumatatu hapatakuwa na “miujiza” kumaliza janga la virusi vya corona, pamoja na kuwepo juhudi za kuharakisha kugundua chanjo inayofanya kazi. 

WHO imehimiza serikali na wananchi kujikita katika kufanya mambo ya msingi, kama vile kupima, kufuatilia maambukizi, kuendeleza kutokaribiana na kuvaa barakoa ili kudhibiti janga hilo, ambayo imevuruga maisha ya kawaida duniani na kuleta mgogoro wenye kuzorotesha uchumi.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kila wiki na Waandishi habari mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema:

“ Kuna idadi fulani ya chanjo ambazo ziko katika hatua ya tatu ya majaribio na sisi sote tuna matumaini kupatikana chanjo kadhaa ambazo zinazofanya kazi kuweza kuwasaidia watu kutoambukizwa."

Aliendelea kusisitiza kwamba “Hata hivyo hakuna miujiza wakati huu – na wala huenda pasiwepo kamwe."

Akiwa Pamoja na mkuu wa idara ya dharura ya WHO Mike Ryan, wakuu hao wamesisitiza kwamba mataifa yote inabidi kuchukua hatua thabiti ya kuwataka watu kufuata mambo ya msingi ya afya ya umma ikiwa ni kukosha mikono, kuvaa barakoa na kutokaribiana ili kudhibiti ugonjwa na kuzuia maambukizo.

Virusi vipya vya corona vimeuwa takriban watu 690,000 na kuambukiza watu wasiopungua milioni 18.1 tangu mlipuko wa ugonjwa COVID-19 kutokea huko Wuhan nchini China mwezi Disemba iliopita, kulingana na takwimu za WHO.

Katika mkutano huo Tedros ametangaza kwamba timu ya waatalamu wa WHO na wa China wanatazamiwa kukamilisha upelelezi wao huo Wuhan na kuanza uchunguzi wa kina juu ya kiini halisi cha mlipuko wa Corona mpya katika mji wa Wuhan.

XS
SM
MD
LG