Badala yake Tedros Adhanom Gebreyesus amesema kuna uwezekano mwaka 2022 kuondoka katika awamu kali ya janga hilo ambapo COVID-19 imekuwa dharura ya afya duniani.
Amesema hilo linaweza kufikiwa iwapo mikakati na zana kama vile upimaji na chanjo vinatumika kwa njia ya kina.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Bodi ya Utendaji, Tedros amesema tangu Omicron kutambuliwa kwa mara ya kwanza zaidi ya wiki tisa zilizopita zaidi ya kesi milioni 80 ziliripotiwa kwa shirika hilo la Umoja wa Mataifa, zaidi ya ilivyoripotiwa mwaka 2020.