Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 10:09

Rais wa Botswanan apatikana kuwa na Covid-19


Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi.
Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi.

Maafisa nchini Botswana wamesema Jumatatu kwamba Rais Mokgweetsi Masisi amejiweka karantini baada ya kugundulika ana virusi vya corona.

Msemaji wa serikali ya Botswana John Dipowe amesema kwamba Masisi amejiweka karantini kwenye makazi yake rasmi baada ya kupata matokeo ya vipimo vya corona.

Dipowe amewahakikishia wananchi kwamba licha ya kugundulika ana virusi vya covid, kiongozi huyo hajaonyesha dalili zozote za maradhi, na kwamba ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari muda wote wa karantini.

Amesema kwamba hatua hiyo imechukuliwa kulingana na kanuni za kiafya kuhusiana na covid-19.Hii ni mara ya kwanza kwa rais Masisi kupatikana na virusi vya corona ingawa hapo awali alijiweka karantini mara kadhaa kama hatua ya tahadhari baada ya watu waliokuwa karibu naye kupatikana na virusi.

Taarifa zimeongeza kusema kwamba makamu wa rais Slumber Tsogwane atakuwa kaimu rais wakati akiwa kwenye karantini.Botswana na Afrika kusini yalikuwa mataifa ya kwanza kutangaza aina mpya ya virusi vya corona vya omicron hapo Novemba na tangu wakati huo maambukizi yameongezeka maradufu ingawa maafisa wa afya wanasema kwamba hayajapelekea watu wengi kulazwa hospitali au vifo.

Wakati huo huo shirika la habari la reuters limesema kwamba wataalamu wa afya wa Afrika kusini wanasema kwamba makali ya omicron huenda yamepunguzwa na watu waliopokea chanjo pamoja na uzoefu wa miili ya watu kutokana na maambukizi ya awali kabla ya omicron kuingia.

XS
SM
MD
LG