Maambukizi ya Omicron yameweka rekodi ya juu sana kuwahi kuripotiwa katika nchi.
Watu 590,000 wamegunduliwa kuambukizwa Omicron Jumatatu pekee, ikiwa ni mara mbili ya idadi ya watu waliogunduliwa kuambukizwa virusi hivyo siku nne kabla.
Maambukizi yamekuwa yakiongezeka mara mbili tangu wiki iliyopita.
Idadi ya maambukizi ni mara mbili ya idadi inayoripotiwa kwingineko duniani tangu janga la Corona lilipotokea kote duniani miaka miwili iliyopita.
Maambukizi ya juu kuwahi kurekodiwa nje ya Marekani, ilikuwa ni nchini India mwezi Mei tarehe 7 mwaka 2021, ambapo watu 414,000 waligunduliwa kuambukizwa.
Ongezeko la maambukizi limepelekea maelfu ya shule kufungwa hnchini Marekani na wanafunzi kulazimika kusomea nyumbani kwa njia ya mtandao.
Kadhalika, idadi ya watoto wanaolazwa hospitali kutokana na Covid imeongezeka. Kwa wastani, watoto 500 walilazwa hospitali kila siku kutokana na Corona, kati ya Desemba tarehe 25 na 31.