Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 09:46

Kasi ya maambukizi ya Omicron duniani imevunja rekodi - WHO


Mkurugenzi wa WHO Tedros Gebreyesus
Mkurugenzi wa WHO Tedros Gebreyesus

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya ulimwenguni, WHO, amesema kwamba zaidi ya visa milioni 15 vya maambukizi ya virusi vya corona, vilivyoripotiwa wiki iliyopita yalisababishwa na kirusi kipya cha Omicron.

Tedros Adhanom Gebreyesus amesema kwamba idadi hiyo ni ya juu Zaidi, kuwahi kuripotiwa ndani ya kipindi cha wiki moja.

Hata hivyo idadi ya vifo bado iko pale pale tangu mwezi Oktoba mwaka jana, ikiwa ni ya wastani wa vifo 48,000.

Ameongeza kuwa ingawa kirusi cha Omicron hakisababishi maambukizi makali kuliko Delta lakini bado kinasalia kuwa hatari na hasa kwa wale ambao hawajapata chanjo.

Tedros pia ameonya kwamba bado kuna njia ndefu kabla ya kufikia lengo la chanjo la asilimia 70 ya watu katika nchi zote ifikapo katikati ya mwaka huu wa 2022.

Marekani ni kati ya nchi zilizoshuhudia ongezeko kubwa zaidi la maambukizi ya kirusi cha Omicron ndani ya kipindi kifufupi mno.

XS
SM
MD
LG