Upinzani na vyama vya wanahabari vimemtaka Moses Kuria kukemewa kutokana kwa kuropoka kwake, wakisema kuwa hafai kushikilia nyadhifa za umma.
Jazba zilizuka wakati Kuria alipokishambulia chombo habari kikubwa cha habari Afrika mashariki cha Media Group (NMG) kinachomilikiwa na Aga Khan.
Katika hafla iliyofanyika hadharani siku ya Jumapili, Kuria aliwatishia kuwafukuza kazi maafisa wa serikali waliopeleka matangazo NMG na kukiuliza chombo hicho cha habari kama ni "chama cha upinzani."
"wizara yoyote ya serikali nikiiona impeleka matangazo kwenye “majukwaa” ya Nation Media ujue umefukuzwa kazi," alisema.
Katika tweet iliyochapishwa kwa lugha ya Kiswahili, aliwataja "makahaba wa Aga Khan."
Pia alidai kuwa waandishi wa habari wa NMG "wamekiri kulazimishwa na wahariri pamoja na utawala kuandika habari zinazoipinga serikali katika mpango uliofadhiliwa na rais wa zamani wa nchi hiyo.
NMG ilisema kuwa ghasia hizo zimetokea baada ya uchunguzi uliotangazwa Jumapili na kituo chake cha NTV kuhusu kashfa zinazohusiana na mpango wa uagizaji bidhaa unaoendeshwa na shirika la serikali lililopo katika wizara ya Kuria.
Wiki hii, Seneta wa upinzani Edwin Sifuna aliwasilisha hoja dhidi ya Kuria, akionya kwamba shambulio dhidi ya chombo kimoja cha habari "mara nyingi husababisha mashambulizi dhidi ya uhuru wa habari kwa ujumla."
Hata hivyo Kuria aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kuwa “hataomba msamaha”
Vyama vya Waandishi wa habari vimejibu matamshi ya waziri huyo kwa hasira, ambaye alizua mjadala mkubwa siku ya Jumatatu wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya mkataba mkubwa ya kibiashara kati ya Kenya na Umoja wa Ulaya.
Muungano wa Wanahabari wa Kenya (KUJ) ulisema "amekuwa ishara ya aibu kwa kitaifa" huku Baraza la Vyombo vya Habari nchini Kenya lilisema matamshi yake ni "tishio la uhuru wa vyombo vya habari na kuharibu taswira ya Kenya duniani kote".
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.
Forum