Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan alisema kuwa katika ziara yake, Kishida atatoa “heshima kwa ushujaa na ustahmilivu wa wananchi wa Ukraine ambao wamesimama kuitetea nchi yao chini ya uongozi wa Zelenskyy, na kuonyesha mshikamano na uungaji mkono usiotetereka kwa Ukraine kama kiongozi wa juu wa Japan na mwenyekiti wa G-7.
Taarifa ya wizara hiyo pia ilisema Kishida ataelezea kupinga mabadiliko ya upande mmoja ya Russia kwa kutumia uvamizi na matumizi ya nguvu.”
Kishida ni kiongozi wa dunia hivi karibuni kufanya ziara katika nchi ya Ukraine iliyo katika vita tangu kuanza Russia ilipoanzisha uvamizi kamili mwezi Februari 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alitangaza Jumatatu kuwa Marekani itatoa msaada dola milioni 350 kwa Ukraine ikiwa ni vifaa na silaha, wakati mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Umoja wa Ulaya wakikamilisha mpango wa kuipatia silaha Ukraine huku wakijaza tena akiba yao ya silaha.
Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.The Associated Press.