Safari ya Xi kuanzia tarehe 20 hadi 22 Machi inajiri baada ya China kuchapisha mwezi uliopita mpango wenye vipengele 12 wa ‘suluhisho la kisiasa kwa ajili ya mzozo wa Ukraine’ na baada ya mwanadiplomasia mkuu wa China kutoa wito wa mazungumzo jana Alhamisi katika mawasiliano ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine.
Mpango huo unatoa wito wa kuwalinda raia na kwa Russia na Ukraine kuheshimu uhuru wa kila mmoja wao.
Hata hivyo, Marekani na NATO wamesema juhudi za Beijing kupatanisha katika mzozo wa Ukraine sio za kuaminika kwa sababu imejizuia kulaani uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, ambao Moscow inauita ‘operesheni maalum ya kijeshi.’