Mapema wiki hii ripoti hiyo imeeleza, manaibu wawakilishi wa baraza la Duma la Russia waliwasilisha mswaada wa kubadilisha kigezo cha umri ili kuandikishwa kwa wanaume jeshini wenye umri wa miaka 21 hadi miaka 30.
Hivi sasa umri unaokubalika ni 18 hadi 27.
Mswaada huo huenda ukapita taarifa imeeleza, na utaanza kutumika Januari.
Ripoti hiyo ilisema wanaume wengi wenye umri wa miaka 18 hadi 21 wanadai kusamehewa ili kuendelea na masomo.
Wahati huohuo Kundi la mamluki la Russia, Wagner linapanga kuandikisha wapiganaji takriban 30,000 ifikapo katikati mwa Mei, amesema mwanzilishi wake Yevgeny Prigozhin Jumamosi.
Katika ujumbe wa sauti uliowekwa kwenye Telegram, kama alivyosema wiki iliyopita, kuwa Wagner imefungua vituo 42 vya uandikishwaji wapiganaji katika miji ya Russia ambapo kwa wastani huandikisha watu kati ya 500 na 800 kwa siku.