Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:39

Wachunguzi wa UN wamezishutumu mamlaka za Russia kwa ukiukaji mbalimbali wa haki za binadamu


Wanajeshi wa Ukraine wakikusanya miili ya raia waliouawa na majeshi ya Russia humo Irpin karibu na Kyiv, Ukraine, March 31, 2022.
Wanajeshi wa Ukraine wakikusanya miili ya raia waliouawa na majeshi ya Russia humo Irpin karibu na Kyiv, Ukraine, March 31, 2022.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamezishutumu mamlaka za Russia kwa mwenendo mbaya wa ukiukaji mbalimbali wa haki za binadamu dhidi ya raia wa Ukraine, ambapo katika matukio mengi, inaweza kupelekea uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Katika ripoti yake ya kwanza ya kina juu ya hali ya Ukraine tangu Russia kuivamia nchi hiyo Februari 24, 2022, wajumbe watatu wa Tume ya Uchunguzi ya Kimataifa kwa Ukraine imehitimisha kuwa “mamlaka nchini Russia zimefanya ukiukaji mbalimbali wa sheria za kimataifa za binadamu na sheria za kimataifa za haki za binadamu, ikiwemo pia uhalifu wa vita wa namna mbalimbali.

Uhalifu wa vita ni pamoja na mashambulizi dhidi ya Ukraine na miundombinu inayohusiana na nishati, mauaji ya kukusudia, mateso na vitendo vya kinyama, kuweka watu kizuizini bila ya sheria, ubakaji na kuwahamisha na kuwaondosha kinyume cha sheria watoto kutoka Ukraine kwenda kwenye Shirikisho la Russia.

“Vita nchini Ukraine vimekuwa na athari za uharibifu katika ngazi mbalimbali,” alisema Erik Mose, mwenyekiti wa tume hiyo. “Vifo vya watu na kutokujali kwa jumla maisha ya raia kunashtusha.

“Idadi ya watu waliokoseshwa makazi au wale wanaotafuta hifadhi nje ya nchi iko juu mno huko Ulaya tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia,” alisema.

Ofisi ya UN kwa ajili ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu inaripoti kuwa zaidi ya watu milioni 5.4 wamekoseshwa makazi ndani ya nchi, na zaidi ya Waukraine milioni 8.1 wamekimbia kama wakimbizi katika nchi jirani za Ulaya.

XS
SM
MD
LG