Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:18

Russia yasema iko tayari kuruhusu upanuzi wa mkataba wa mauzo ya nafaka

Rais wa Russia Vladimir Putin akihudhuria sherehe za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake huko Kremlin Moscow, Machi 8, 2023.REUTERS
Rais wa Russia Vladimir Putin akihudhuria sherehe za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake huko Kremlin Moscow, Machi 8, 2023.REUTERS

Russia ilisema Jumatatu iko tayari kuruhusu upanuzi wa mkataba wa mauzo ya nafaka wa Ukraine ambao umesaidia kupunguza bei za chakula duniani lakini kwa siku 60 pekee.

Russia ilisema Jumatatu iko tayari kuruhusu upanuzi wa mkataba wa mauzo ya nafaka wa Ukraine ambao umesaidia kupunguza bei za chakula duniani lakini kwa siku 60 pekee.

Ujumbe wa Russia katika mazungumzo na maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa ulielezea mazungumzo hayo Jumatatu kuwa ya kina na ya wazi lakini wakasema Russia inataka kuona mafanikio yanayoonekana kwenye makubaliano sambamba ya mauzo ya nje ya Russia kabla ya mkataba wa nafaka wa Ukraine kuandikwa upya.

Mpango wa Nafaka wa Black Sea unaruhusu Ukraine mojawapo ya wazalishaji wakuu wa nafaka duniani kusafirisha kwa usalama chakula na mbolea kutoka bandari tatu za nchi hiyo.

Mkataba huo wa nafaka ulisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki Julai mwaka jana ili kusaidia kupunguza mzozo wa chakula duniani na uliongezwa kwa siku 120 mwezi Novemba. Muda wa nyongeza hiyo unatarajiwa kuisha siku ya Jumamosi.

XS
SM
MD
LG