Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 01, 2024 Local time: 22:55

Waziri Mkuu mpya wa Haiti ziarani Marekani


Waziri Mkuu mpya wa Haiti Garry Conille.
Waziri Mkuu mpya wa Haiti Garry Conille.

Kiongozi mpya wa Haiti aliwasili nchini Marekani siku ya Jumamosi kwa ziara iliyopangwa kujumuisha mikutano na taasisi za fedha za kimataifa pamoja na afisa wa White House, ofisi yake na msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa alisema.

Ziara ya Waziri Mkuu Garry Conille, anayeongoza serikali ya mpito ya nchi hiyo, na maafisa wengine inajiri siku chache baada ya polisi wa Kenya hatimaye kuwasili Haiti iliyokumbwa na ghasia, kama sehemu ya ujumbe uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu kusaidia kuleta utulivu katika taifa hilo la Karibean, linaloongozwa na magenge yenye nguvu.

Washington imeahidi ufadhili mkubwa kwa ujumbe huo unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, lakini haitatuma vikosi vyake.

Conille atakutana na Naibu Mkuu wa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Jon Finer siku ya Jumatatu, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa alisema.

Conille, akiandamana na mawaziri wake wa uchumi na mambo ya nje pamoja na maafisa wengine, pia watafanya "mikutano muhimu ya kikazi" na wakuu wa taasisi za fedha za kimataifa, kulingana na ofisi yake.

Pia watatembelea ubalozi wa Haiti mjini Washington na kusafiri hadi New York, ilisema.

Haiti kwa muda mrefu imekuwa ikikumbwa na ghasia za magenge, lakini hali ilizidi kuwa mbaya zaidi mwishoni mwa Februari wakati makundi yenye silaha yalipoanzisha mashambulizi yaliyopangwa katika mji mkuu, Port-au-Prince, yakisema yalitaka kumpindua waziri mkuu wa wakati huo Ariel Henry.

Henry alitangaza mapema mwezi Machi kwamba atajiuzulu na kukabidhi mamlaka ya utendaji kwa baraza la mpito, ambalo lilimtaja Conille kama waziri mkuu wa muda wa nchi hiyo mnamo Mei 29.

Forum

XS
SM
MD
LG