Kwa jumla, hukumu 1,278 zilitolewa, huku zaidi ya asilimia 95 ya washtakiwa wakihukumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali hadi kuwashambulia maafisa wa polisi.
Watu mia sita tayari wamefungwa jela.
“Ilikuwa muhimu sana kuchukuliwa hatua ambayo ni thabiti na ya kimpangilio,” Waziri wa Sheria Eric Dupond-Moretti alikiambia kituo cha radio cha RTL. “Ilikuwa muhimu turejeshe utulivu wa taifa.”
Ghasia mbaya zaidi za mjini nchini Ufaransa tangu 2005 zilianza Juni 27 baada ya afisa wa polisi kumpiga risasi na kumuua kijana wa miaka 17 mwenye asili ya Afrika Kaskazini wakati aliposimama kwenye alama ya barabarani magharibi ya Ufaransa, katika tukio lililorekodiwa na mpita njia.
Ghasia hizo zilidhibitiwa baada ya siku nne za usiku zilizokuwa na mapambano mabaya shukran kwa upelekaji majeshi ya usalama takriban 45,000, wakiwemo polisi maalum na magari yenye silaha.
alikuwa ameongoza wito kwa mahakama kutoa adhabu kali kama fundisho, huku mahakama nyingine zikiwa wazi siku za wikiendi zilizokuwa na mapambano kusikiliza mrundikano wa kesi.
Washukiwa wengi walipelekwa moja kwa moja mbele ya Mahakama na baadhi ya mawakili wa utetezi wameeleza wasi wasi wao kuhusu utendaji haki wa mchakato wa mahakama na matumizi ya hukumu nzito za kifungo.
Wastani wa umri kwa zaidi ya watu 3,700 waliokamatwa ulikuwa miaka 17, huku wale waliokuwa watoto wadogo wakifishwa katika mahakama za watoto.
Idadi ya watu waliohukumiwa kifungo imevuka ile ya mwaka 2005 wakati palipotokea ghasia kubwa za mwisho huku watu karibu 400 wakihumiwa kifungo jela.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.
Forum