Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:06

Watu 6 wauawa kufuatia mlipuko wa bomu mpaka wa Kenya na Somalia


Bomu laua watu 6 mpaka wa Kenya na Somalia
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:49 0:00

Bomu laua watu 6 mpaka wa Kenya na Somalia

Polisi wa Kenya wamesema leo Jumatatu watu sita wameuawa  wakati basi dogo la abiria lilipoharibiwa na bomu la kutegwa ardhini huko kaskazini mashariki mwa nchi wakati wa shambulio la kuvizia lililofanywa na watu wenye silaha karibu na mpaka wa Somalia.

Washambuliaji walifyatua risasi kwenye basi hilo lenye viti 14 baada ya kukanyaga kilipuzi takriban kilomita nane kutoka mji wa Mandera kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.

Ripoti ya polisi kuhusu tukio hilo imesema kwamba “Kikosi cha doria ambacho kilikuwa kwa miguu na karibu na eneo hilo, kilijibu na kukabiliana na washambuliaji ambao walikimbia kuelekea upande wa Somalia”.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa washambuliaji walitumia bunduki na maguruneti ya kurushwa kwa roketi wakati wa shambulio hilo.

Abiria wengi walinusurika katika shambulio hilo wakiwa na majeraha ya viwango tofauti, ripoti ya polisi imesema.

Eneo la Mandera linakabiliwa na uvamizi kwenye mkapa wake mrefu na Somalia na wenye njia za vichakani, ambapo kundi la wanamgambo wa Al Shabaab linadhibiti maeneo ya vijijini na mamlaka ya serikali kuu katika maeneo ya mbali ikiwa dhaifu.

XS
SM
MD
LG