Vikosi vinavyomuunga mkono waziri mkuu Jumanne vilipiga kambi karibu ya ikulu ya rais, na hivyo kuzusha hali ya taharuki katika mji mkuu Mogadishu.
Msemaji wa serikali ya Somalia, Mohamed Ibrahim Moalimu na mshauri mkuu wa Roble, ameandika kwenye Twitter kuwa waziri mkuu alizungumza na Molly Phee, waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika, na walizungumza kuhusu hali ya kisiasa nchini Somalia, usalama na uchaguzi.
Jumatatu, rais Mohamed alimsimamisha kazi waziri mkuu kwa tuhuma za ufisadi, hatua ambayo waziri mkuu ameikemea kuwa ni jaribio la mapinduzi.