Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:30

Watu 6 wauawa na wanamgambo wa Al Shabaab nchini Kenya


Afisa wa vikosi vya usalama vya Kenya akitembea karibu na kituo cha polisi kilichoharibiwa baada ya shambulio la Al Shabaab Kaunti ya Garissa, Januari 13, 2020. Picha ya AP
Afisa wa vikosi vya usalama vya Kenya akitembea karibu na kituo cha polisi kilichoharibiwa baada ya shambulio la Al Shabaab Kaunti ya Garissa, Januari 13, 2020. Picha ya AP

Watu 6 wameuawa na nyumba kuchomwa moto katika shambulio baya leo  Jumatatu  linaloshukiwa limefanywa na   wanamgambo wa Al Shabaab katika eneo la pwani ya Kenya linalopakana na Somalia, polisi na  maafisa wa serikali wamesema.

Mwanamme mmoja alikatwa kichwa na wengine watano kupigwa risasi au kuchomwa moto hadi kufa katika shambulizi kwenye kijiji kimoja katika kaunti ya Lamu takriban kilomita 420 kusini mashariki mwa mji wa Nairobi, polisi wamesema.

Kamshina wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema washambuliaji wanashukiwa ni wanajihadi wa kundi la Al Shabaab lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda, lenye makao yake nchini Somalia.

Polisi wamesema washambuliaji walimchoma kisu na kumkata kichwa mzee wa eneo hilo na kuichoma nyumba yake, na kumuua mtu mwengine ambaye mwili wake ulipatikana kando ya barabara karibu na hapo.

Maiti za wanaume wengine wanne zilichomwa moto kiasi cha kutotambulika zilipatikana katika eneo jingine, kulingana na ripoti ya polisi ambayo shirika la habari la AFP imeiona.

XS
SM
MD
LG