Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:54

Msemaji wa serikali ya Somalia ajeruhiwa katika shambulizi


Gari alimokuwa msemaji wa serikali ya Somalia Mohamed Ibrahim Moalimuu ambalo lililipuliwa mjini Mogadishu, Jan. 16, 2022.
Gari alimokuwa msemaji wa serikali ya Somalia Mohamed Ibrahim Moalimuu ambalo lililipuliwa mjini Mogadishu, Jan. 16, 2022.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga katika mji mkuu wa Somalia amemjeruhi msemaji wa serikali na mwanahabari wa zamani Mohamed Ibrahim Moalimuu.

Mashahidi waliiambia Sauti ya Amerika kwamba mshambuliaji wa kujitoa mhanga alikimbia kuelekea kwenye gari la Moalimuu katikati mwa Mogadishu na kutegua fulana iliyokuwa na Kilipuzi.

Moalimuu alipata majeraha kwenye mkono na mguu kutokana na vipande vya vilipuzi kutoka kwenye bomu hilo.

Kundi la wanamgambo wa Somalia al-Shabab mara moja lilidai kuhusika na shambulio hilo.

Moalimuu amenusurika walau mashambulizi matatu ya awali ya al-Shabab, na alitweet akisema Ilikuwa ni bahati kuepuka hili baada ya kunusurika moja mwaka 2016.

XS
SM
MD
LG