Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:45

Watoto wawili wauawa na wengine 11 wajeruhiwa kwa kisu Uingereza


Takriban watu nane wakiwemo watoto wamejeruhiwa katika shambulio la kisu huko Kaskazini Mahgaribi mwa Uingereza. Picha na AP
Takriban watu nane wakiwemo watoto wamejeruhiwa katika shambulio la kisu huko Kaskazini Mahgaribi mwa Uingereza. Picha na AP

Mtoto wa kiume aliyekuwa na kisu amewashambulia watoto waliokuwa katika darasa la kucheza dansi na yoga Kaskazini Magharibi mwa Uingereza siku ya Jumatatu.

Katika shambilio hilo watoto wawili waliuwawa na wengine 11 kujeruhiwa katika shambulio la “kikatili” lililowafanya watoto waliokuwa wakitiririka damu kkukimbia kutokana hofu kwenda barabarani, polisi na mashuhuda walisema.

Kijana mwenye umri wa miaka 17 alikamatwa kwa kushukiwa na mauaji na jaribio la kuua katika shambulio lililotokea Southport, mji wa pwani jirani na Liverpool, polisi wa Merseyside walisema.

Azma ya tukio hilo haijulikani, lakini polisi wanasema wapelelezi hawalichukulii shambulio kuwa linahusiana na ugaidi.

Watoto tisa wamejeruhiwa, sita kati yao ni mahututi. Watu wazima wawili walijeruhiwa wakati walipokuwa wakijaribu kuwalinda watoto hao, pia wako katika hali mbaya, polisi wamesema .

Forum

XS
SM
MD
LG