Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 09:54

Watu watano wauawa na waasi wa ADF mashariki mwa DRC


Wanajeshi wa DRC wakifanya doria katika kijiji cha Mwenda kufuatia shambuluo la hivi karibuni la ADF. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP
Wanajeshi wa DRC wakifanya doria katika kijiji cha Mwenda kufuatia shambuluo la hivi karibuni la ADF. Picha na ALEXIS HUGUET / AFP

Waasi wenye uhusiano na kundi la Islamic State waliwauwa watu watano mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika shambulio Jumatano, vyanzo vya eneo hilo vimeiambia AFP.

“Niliona na macho yangu watu watano waliokatwa vichwa,” mkazi moja aliiambia AFP.

Mkazi huyo aliona miili ya watu hao kwenye kituo cha huduma ya afya cha karibu ambako waasi hao walishambulia katika wilaya ya Beni ya jimbo la Kivu Kaskazini.

Chanzo kingine kimethibitisha idadi ya vifo vya watu watano na kulilaumu kundi la wanamgambo la ADF kuhusika na shambulio hilo, ambalo lilitangaza kujiunga na IS.

“ADF kwa mara nyingine wametuacha katika maombolezo. Wameua waendesha baiskeli watano waliokuwa wakienda sokoni,” alisema Leo Siviwe, mkuu wa wilaya ambako kituo hicho cha afya kipo.

Kundi la ADF, lenye wapiganaji wengi Waislamu raia wa Uganda, limeimarisha uwepo wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika miongo mitatu iliyopita, na kuua maelfu ya raia.

Forum

XS
SM
MD
LG