Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:48

Mashambulizi ya anga ya Israel yaua watu 9 Ukanda wa Gaza


Wapalestina wakitizama jinsi shambulizi la anga la Israel lilivyoharibu makazi ya wakimbizi huko Rafah, Mei 27, 2024. Picha ya AP
Wapalestina wakitizama jinsi shambulizi la anga la Israel lilivyoharibu makazi ya wakimbizi huko Rafah, Mei 27, 2024. Picha ya AP

Maafisa wa afya wa Palestina wamesema mashambulizi ya anga ya Israel yaliua watu tisa Jumatano katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Shambulio moja la anga lililenga nyumba moja huko Al-Zawyda na kuua watu wanane. Lingine lililenga kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, na kuua mtu mmoja.

Maafisa wanasema shambulio lingine la anga la Israel lililenga kambi hiyo hiyo na kuua watu 23 siku ya Jumanne.

Jeshi la Israel linasema lilishambulia ngome 25 katika Ukanda wa Gaza katika mashambulizi ya anga Jumanne.

Hata hivyo, shambulio tofauti la Israel liliua watu wawili huko Rafaf Jumatano, kulingana na wanaotoa matibabu katika eneo hilo. Wakazi wameeleza kuwa nyumba kadhaa ziliharibiwa na vifaru vya Israel kaskazini mwa mji wa Rafah.

Jeshi la Israel lilifanya pia mashambulizi ya anga Jumatano kusini mwa Lebanon katika mashambulizi ya hivi karibuni yanayowalenga wanamgambo wa Hezbollah.

Forum

XS
SM
MD
LG