Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 02:32

Kenya: Polisi wachunguza vifo vya watoto 17 waliofariki kutokana na ajali ya Moto


Wazazi na wananchi katika jamii wamekusanyika nje ya shule ya Hillside Endarasha Academy huko kaunti ya Nyeri Parents Septemba 6, 2024 baada ya moto kuua watoto 17.
Wazazi na wananchi katika jamii wamekusanyika nje ya shule ya Hillside Endarasha Academy huko kaunti ya Nyeri Parents Septemba 6, 2024 baada ya moto kuua watoto 17.

Watoto 17 wamefariki katika moto ulioteketeza bweni la shule yao ya msingi usiku wa kuamkia Ijumaa, katikati mwa Kenya, polisi ilisema.

Moto huo ulitokea katika shule ya Hillside Endarasha Academy iliyoko kwenye kaunti ya Nyeri ulianza Alhamisi usiku, polisi walisema, wakibainisha kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na umri wa wastani wa waathirika ni takriban miaka tisa.

Shule hiyo, ambayo ina wanafunzi wapatao 800 wenye umri wa miaka mitano hadi 12, iko katika eneo la vijijini, takriban kilomita 170 kaskazini mwa mji mkuu Nairobi.

“Kuna vifo 17 na wengine kadhaa wamejeruhiwa, wakiwemo 16 waliojeruhiwa vibaya, na wamekimbizwa hospitali,” alisema msemaji wa polisi, Resila Onyango aliliambia shirika la habari la AFP.

“Miili iliyopatikana kwenye eneo la tukio imeungua kiasi cha kutotambulika,” aliongeza.

“Miili mingine huenda ikapatikana” mara baada ya ukaguzi wa eneo la tukio kukamilika, kulingana na msemaji huyo.

Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto huo, aliongeza.

Televisheni ya Citizen TV ilionyesha picha za paa la bati lililokuwa limeungua na kujikunja.

Kulingana na Tume ya Jinsia na Usawa ya Kenya, ambayo inadai uchunguzi wa kina, taarifa za awali zinaonyesha kuwa bweni hilo lilikuwa "limejaa kupita kiasi, kinyume na kanuni za usalama."

Akiliita tukio hilo kuwa "habari ya kusikitisha," Rais William Ruto, ambaye kwa sasa yuko Beijing katika mkutano wa China na Afrika, alitoa rambirambi zake. "Mawazo yetu yako na familia za watoto waliopoteza maisha" katika "janga hili," alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa X.

Bwana Ruto aliongeza kuwa aliwataka maafisa "kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hili la kutisha" na kuahidi kwamba wahusika "watawajibishwa."

Ijumaa, mwandishi wa habari wa AFP alishuhudia wazazi wapatao mia moja walikuwa wamekusanyika mbele ya shule hiyo, wakisubiri kwa wasiwasi kupata habari kuhusu watoto wao.

Forum

XS
SM
MD
LG