Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 18:10

Mwanariadha wa mbio ndefu Rebecca Cheptegei raia wa Uganda amefariki


Mwanariadha Rebecca Cheptegei amefariki kutokana na majeraha ya moto
Mwanariadha Rebecca Cheptegei amefariki kutokana na majeraha ya moto

Vyombo vya habari vya Kenya na Uganda vimeripoti Cheptegei mwenye miaka 33 alishiriki katika michezo ya Olimpiki ya Paris

Mwanariadha wa mbio za ndefu raia wa Uganda, Rebecca Cheptegei amefariki dunia, maafisa wa hospitali wamesema leo Alhamisi, siku chache baada ya kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na mpenzi wake.

Vyombo vya habari vya Kenya na Uganda vimeripoti kuwa Cheptegei, mwenye miaka 33 ambaye alishiriki katika michezo ya Olimpiki ya Paris, alipata majeraha ya moto kwa zaidi ya asilimia 75 mwilini mwake katika shambulio lililotokea nchini Kenya siku ya Jumapili, na kumfanya kuwa mwanariadha wa tatu kuuawa nchini humo tangu Oktoba 2021.

Tumefahamu kuhusu kifo cha kusikitisha cha mwanariadha wetu wa Olimpiki Rebecca Cheptegei, kufuatia shambulio baya lililofanywa na mpenzi wake, Donald Rukare, rais wa Kamati ya Olimpiki ya Uganda, aliandika kwenye mtandao wa X.

Mwenyezi mungu ampumzishe kwa amani na tunalaani vikali ukatili dhidi ya wanawake. Hiki kilikuwa kitendo cha kikatili na kisicho na maana ambacho kimesababisha kumpoteza mwanariadha mkubwa.

Forum

XS
SM
MD
LG