Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:41

Wapalestina waliojeruhiwa wawasili hospitalini Khan Yunis


Familia zikitorokea mashambulizi katika Ukanda wa Gaza.
Familia zikitorokea mashambulizi katika Ukanda wa Gaza.

Israel ilifanya mashambulizi mapya Jumatano katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah, ambako vikosi vyake vinapambana na wapiganaji wa Hamas, baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kujadili shambulio baya lililosababisha hasira duniani kote.

Licha ya kuongezeka kwa wasiwasi juu ya idadi ya raia waliouawa katika vita vyake dhidi ya Hamas, Israel haijaonyesha dalili za kubadili mweleekeo na juhudi za kimataifa za kupata sitisho la mapigano ambalo limekwama.

Waandishi wa habari wa AFP huko Rafah wameripoti mashambulizi mapya mapema Jumatano, saa kadhaa baada ya mashahidi na vyanzo vya usalama vya Palestina kusema makombora ya Israeli yalipenya katikati ya mji.

"Watu wako ndani ya nyumba zao kwasababu mtu yeyote atakayetoka nje atapigwa na ndege zisizo na rubani za Israel," alisema mkazi Abdel Khatib.

Rais wa Marekani Joe Biden ameionya Israel dhidi ya kuanzisha operesheni kubwa ya kijeshi huko Rafah, lakini utawala wake ulisisitiza Jumanne kwamba Israel haijavuka mipaka yake.

"Hatujaona wakiivamia Rafah," alisema msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani John Kirby.

Afisa wa ulinzi wa raia katika Gaza inayoongozwa na Hamas alisema shambulio la Israel kwenye kambi ya wakimbizi magharibi mwa Rafah Jumanne liliwauwa watu 21, baada ya shambulio kama hilo mwishoni mwa wiki kusababisha hasira duniani na kusababisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Jeshi la Israel lilipinga madai kwamba lilifanya shambulio la Jumanne katika eneo lililotengwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

"Jeshi la Israel halikushambulia eneo la kibinadamu huko Al-Mawasi," jeshi lilisema katika taarifa, likimaanisha eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajili ya watu waliokimbia makazi yao huko Rafah kupata hifadhi.

Forum

XS
SM
MD
LG