Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:43

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wakutana Brussels


Waziri mkuu wa Palestina Mohammad Mustafa alipokaribishwa na Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel huko Brussels, Mei 26, 2024. Picha na REUTERS/JohannaGeron
Waziri mkuu wa Palestina Mohammad Mustafa alipokaribishwa na Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel huko Brussels, Mei 26, 2024. Picha na REUTERS/JohannaGeron

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya – EU wamekusanyika Brussels kwa mkutano Jumatatu kujadili uvamizi wa Russia nchini Ukraine na hali ya usalama huko Mashariki ya Kati.

Umoja wa Ulaya unalenga kukubaliana kimsingi kushinikiza kuhusu hali ya kwenye mpaka huko Rafah mji uliopo kusini mwa Ukanda wa Gaza unaopakana na Misri, mkuu wa sera za mambo ya nje katika EU, Josep Borell amesema.

Umoja huo unafikiria kufufua msaada wa Umoja wa Ulaya wa Mpakani – EUBAM kwa Rafah, ambao haujafanya kazi tangu mwaka 2007, wakati kundi la wanamgambo wa Palestina, Hamas lilipokamata udhibiti wa Gaza.

Kivuko cha Rafah ni njia kuu ya kuingiza misaada kutokea Misri, na kimefungwa tangu majeshi ya Israel yalipochukua udhibiti wa Gaza takriban wiki tatu zilizopita.

Forum

XS
SM
MD
LG