Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 03:24

Mashambulizi ya anga ya Israel yaua watu 35 katika mji wa Rafah, wamesema maafisa wa Gaza


Wapalestina wakagua uharibifu wa nyumba zao baada ya shambulio la anga la Israel huko Rafah, Mei 22, 2024. Picha ya AFP
Wapalestina wakagua uharibifu wa nyumba zao baada ya shambulio la anga la Israel huko Rafah, Mei 22, 2024. Picha ya AFP

Jeshi la Israel linatathmini tukio katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza baada ya maafisa wa afya kusema kulikuwa na mashambulizi ya Israel ambayo yameua raia 35 jana Jumapili.

Israel imesema shambulizi katika ujirani wa Tel Al-Sultan huko Rafah , ambalo limemuua mkuu wa wafanyakazi wa Hamas kwa Ukingo wa Magharibi na afisa mwingine mwandamizi, lilifanyika kwa kutumia silaha zenye shabaha ya uhakika. Lakini wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza imesema shambulizi limesababisha mahema kushika moto katika eneo ambalo linawahifadhi watu wasiokuwa na makazi.

Darzeni ya watu pia walijeruhiwa, maafisa wamesema, na Jamii ya Mwezi Mwekundi ya Palestina inatarajia idadi ya vifo itaongezeka.

Mapema Jumapili, Hamas ilirusha mfululizo wa roketi wakilenga kiunga cha biashara cha Tel Aviv. Ilikuwa ni shambulizi la kwanza katika miezi kadhaa, na kuonyesha uthabiti kutoka kwa wanamgambo wa Palestina katika miezi minane ya vita kati ya Israel na Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG