Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:17

Misri yakubali kupelekwa magari ya misaada Gaza


Misri imesema Ijumaa imekubali kupeleka magari ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kupitia kwenye kivuko kikuu cha Israel na kuingia Gaza.

Lakini bado haiko wazi kama yataweza kuingia katika eneo ambalo mapigano yanaendelea katika mji wa kusini wa Rafah huku mashambulizi ya Israel yakisambaa huko.

Wakati huo huo, miili ya mateka watatu zaidi waliouawa Oktoba 7 imegunduliwa wakati wa usiku huko Gaza, jeshi la Israel limesema Ijumaa. Mkuu wa Idara ya Ujasusi (CIA) alikutana mjini Paris na maafisa wa Israel na Qatar, akijaribu kufufua mashauriano kwa ajili ya sitisho la mapigano na kuachiliwa kwa mateka.

Mzozo wa kibinadamu huko Gaza umesambaa wakati UN na mashirika mengine ya misaada yanasema kupeleka chakula na bidhaa nyingine huko kumeshuka sana tangu mashambulizi ya Israel kwa Rafah yalipoanza zaidi ya wiki mbili zilizopita. Ijumaa, mahakama ya juu ya UN – Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) – imeiamuru Israel kusitisha mashambulizi huko Rafah, ingawaje Isreal huenda isitekeleze amri hiyo.

Katika ya tatizo hilo kuna vivuko viwili vikuu ambavyo magari takriban 300 ya misaada kwa siku imekuwa ikiingia Gaza kabla ya mashambulizi kuanza.

Wanajeshi wa Israel walikikamata kivuko cha Rafah kuingia Misri, ambacho tangu wakati huo kimekuwa hakifanyi kazi. Kivuko cha karibu cha Kerem Shalom kati ya Israel na Gaza kimebaki wazi, na Israel inasema imekuwa ikipeleka mamia ya magari kwa siku kuingia huko. Lakini wakati magari ya kibiashara yamefanikiwa kuvuka, UN inasema haiwezi kiufika Kerem Shalom kuchukua misaada wakati ikiingia kwasababu ya mapigano katika eneo hilo inafanya hali iwe ya hatari sana.

Matokeo yake, UN inasema imepokea magari 143 tu kwenye kivuko katika muda wa siku 19 zilizopita. Mamia ya magari ya mizigo yamekaa upande wa Gaza wa kivuko bila ya kurejeshwa, kwa mujibu wa maafisa wa Israel, ambao wanasema wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wana ukomo wao na ndiyo wa kulaumiwa. UN na mashirika mengine ya misaada yalitegemea idadi ndogo ya magari kuingia kila siku kupitia kivuko hicho cha upande wa kaskazini mwa Gaza na kwenye gati ambayo imejengwa na Marekani kufikisha misaada kwa njia ya bahari.

Makundi ya kibinadamu yanajitahidi kupata chakula kukipeleka kwa Wapalestina huku baadhi ya watu 900,000 wamekimbia Rafah, wamesambaa kote katikati na kusini mwa Gaza. Wafanyakazi wa misaada wameonya kuwa Gaza inakaribia kukumbwa na njaa. UNRWA shirika kuu la Umoja wa Mataifa katika juhudi za kibiandamu, limelazimika kusitisha usambazaji chakula katika mji wa Rafah kwasababu limeishiwa na bidhaa.

Tangazo la Misri linaonekana kusuluhisha kikwazo cha kisiasa katika upande mmoja wa mpaka.

Israel inasema imekiweka kivuko cha Rafah wazi na kuitaka Misri kuratibu katika upelekaji wa misafara ya misaada kupitia huko. Misri imekataa, ikikhofia kuwa Israel itafanya iwe ni jambo la kudumu, na kuwataka Wapalestina kuchukua tena jukumu la kituo hicho. White House imekuwa ikiishinikiza Misri kuanza tena mtiririko wa usafiri wa magari ya mizigo.

Katika mazungumzoya simu na Rais wa Marekani, Joe Biden siku ya Ijumaa, Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi alikubali kuruhusu magari iliyobeba misaada ya kibinadamu na mafuta kwenda kwenye kivuko cha Kerem Shalom mpaka suluhisho lipatikane kuhusu kivuko cha Rafah, ofisi ya el-Sissi imesema katika taarifa.

Lakini bado haiko wazi kama UN itakuwa na uwezo wa kupata magari ya ziada ya mizigo kuingia kutoka Misri.

UNRWA haikujibu maombi ya kutoa maoni yao. Katika mtandao wa kijamii wa X siku ya Alhamisi, Imesema “Tunaweza kuanza usambazaji chakula huko Rafah, kesho kama kivuko kitafunguliwa tena na tutapewa njia salama.”

Mercy Corps, kundi la misaada linalofanya shughuli zake huko Gaza, limesema katika taarifa ya Ijumaa kwamba mashambulizi yamesababisha “kufunguwa kwa vivuko viwili ….ambavyo ni muokozi wa maisha” kwa misaada na “vimesabaisha mfumo wa kibinadamu kusimama.”

“Kama mabadiliko makubwa hayatatokea, ikiwa ni pamoja na kufungua vivuko kwa usalama ili kuongeza misaada katika maeneo haya, tunakhofia kwamba wimbi la vifo itakuwa ndiyo matokeo, huku watu wakifa kwasababu ya njaa, ukosefu wa maji safi na huduma za usafi wa vyoo, na kusambaa kwa magonjwa katika maeneo ambako kuna huduma chache za afya,” imesema.

Mapigano yanaonekana kusambaa huko Rafah. Walioshuhudia wamesema upigaji mabomu umeongezeka Ijumaa katika sehemu za mashariki mwa mji, karibu na Kerem Shalom, lakini mashambulizi pia yalikuwa yakifanyika katika wilaya za katikati, kusini na magharibi karibu na kivuko cha Rafah.

Viongozi wa Israel wamesema lazima wawaondoa wapiganaji wa Hamas kutoka Rafah ili kukamilisha kulisambaratisha kundi hilo baada ya shambulizi la kigaidi la Oktoba 7.

Wanamgambo wanaoongozwa na Hamas wameua watu 1,200, wengi wao raia na kuwateka takriban wengine 250 katika shambulizi la Oktoba 7. Takriban nusu ya mateka wameachiliwa tangu wakati huo, wengi kwa kubadilishana na wafungwa wa Palestina wanaoshikiliwa na Israel wakati wa wiki moja ya sitisho la mapigano mwezi Novemba mwaka jana.

Kampeni ya Israel ya mabomu na mashambulizi huko Gaza imeua zaidi ya Wapalestina 35,800 na kujeruhi wengine zaidi ya 80,200, Wizara ya Afya ya Gaza imesema Ijumaa. Hesabu yake haitofautishi kati ya raia na wapiganaji.

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wakati wa usiku wamegundua miili ya watu watatu waliouawa katika shambulizi la Oktoba 7 na hatimaye kuchukuliwa ndani ya Gaza na kuhesabiwa miongoni mwa mateka.

Miili ya Hanan Yablonka, Michel Nisenbaum, na Orion Hernandez Radoux iligunduliwa katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa Gaza, ambako wanajeshi wa Israel wamekuwa wakipigana kwa wiki moja iliyopita na wanamgambo wa Hamas, jeshi limesema.

Tangazo limekuja chini ya wiki moja baada ya jeshi kusema limegundua katika eneo hilo hilo miili ya mateka watatu wa Israel ambao waliuawa Oktoba 7.

Israel inseam mateka 100 bado wanashikiliwa huko Gaza, amoja na miili ya watu 39 zaidi, wakati miili 17 ya mateka imepatikana.

Kundi linalowakilisha familia za mateka limesema miili hiyo imerejeshwa kwa familia zao kwa mazishi. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi ina wajibu wa kufanya kila kitu kuwarejesha wale walioteka, wote waliouawa na walio hai.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametuma salaam za rambi rambi kwa familai ya Hernandez-Radouc, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Mexico, akisema Ufaransa bado ina nia ya dhati ya kusaidia kuachiliwa kwa mateka.

Mkurugenzi wa CIA Bill Burns alikutana mjini Paris siku ya Ijumaa na maafisa wa Israel na Qatar katika mazungumzo yasiyo rasmi yaliyolenga kuwapata mateka na mashauriano ya sitisho la mapigano kurejea kwenye meza, afisa wa Marekani amesema, akiongea katika misingi ya kutotajwa jina.

Burns ana mawasiliano ya karibu na maafisa wa Misri, kama Qatar ambao wamekuwa ni wapatanishi wa Hamas, afisa wa Marekani amesema.

Mazungumzo ya sitisho la mapigano yamesimama mwanzoni mwa mwezi baada ya msukumo mkubwa uliofanywa na Marekani na wapatanishi wengine kutaka kufikiwa kwa makubaliano, kwa matumaini ya kuepuka mpango wa Israel wa uvamizi katika mji wa kusini wa Rafah. Mazungumzo yalijikita zaidi katika suala kuu: Madai ya Hamas kupata dhamana kwamba vitamalizika, na wanajeshi wa Israel wataondoka kabisa kutoka Gaza kwa makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka wote, dai ambalo Israel imelikataa.

Forum

XS
SM
MD
LG