Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 02:23

Maafisa wa UN waonya msaada wa kibinadamu unakwisha huko Gaza


Wapalestina wanaokimbia Rafah kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Israel katika mji huo.
Wapalestina wanaokimbia Rafah kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Israel katika mji huo.

Malori matatu pekee ya WHO yaliyobeba misaada yameingia katika mji wa Rafah uliozingirwa tangu uvamizi wa Israel ulipoanza

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameonya msaada wa dawa na usambazaji wa mafuta huko Gaza unakwisha wakati wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakihangaika kutoa huduma za kuokoa maisha kwa idadi kubwa ya wagonjwa na majeruhi.

Vifaa vya matibabu na vifaa vinavyotumia mafuta vinaendelea kupungua sana”, msemaji wa Shirika la Afya Duniani Dr. Margaret Harris aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva Jumanne. Alisema ni malori matatu pekee ya WHO yaliyobeba misaada yameingia katika mji wa Rafah uliozingirwa tangu uvamizi wa Israel ulipoanza mapema mwezi Mei.

“Tuna malori 60 ya usambazaji ya WHO yanasubiri katika eneo la Al-Arish, hayawezi kuvuka kuingia Rafah kutokana na mpaka kufungwa” alisema. Mafuta ni muhimu sana, alisema akieleza kuwa wastani wa lita 200,000 kwa siku zinahitajika kuendesha huduma za afya katika hospitali 14 zinazofanya kazi rasmi huko Gaza.

“Tumefanikiwa kupata lita 60,000 kwa siku. Baadhi ya siku hakuna. Kwa hivyo, hospitali zote zinataabika sana na kufanya maamuzi juu ya kile wanachoweza kufanya, hasa katika mji wa Rafah ambapo hospitali ya Emirati pekee ndiyo inayoendelea kufanya kazi.

Forum

XS
SM
MD
LG