Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 13:39

Changamoto za ulimwengu zinaongezeka na Afya inazorota; Anasema Guterres


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Mamilioni ya watu Sudan na Gaza wako hatarini kufa sio tu kutokana na risasi na mabomu lakini majeraha yasiyotibiwa na magonjwa

Baraza Kuu la 77 la Shirika Afya Duniani lilifungua kikao chake cha kila mwaka cha wiki nzima Jumatatu kwa maelezo ya kawaida, wakati wajumbe walikuwa wanakabiliwa na jukumu la kuweka sera za afya kwa mwaka ujao huku kukiwa na changamoto kubwa kwa ustawi wa ulimwengu kutokana na migogoro mingi ambayo, katika baadhi ya maeneo, ilitishia kufuta miongo kadhaa ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameliambia baraza hilo kwa njia ya video kutoka New York nchini Marekani, kwamba dunia inakabiliwa na matatizo na kwamba afya ya ulimwengu inataabika “kuanzia machafuko ya hali ya hewa hadi kuongezeka kwa umaskini na ukosefu wa usawa, na kuzidisha migogoro”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. February 19, 2024.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. February 19, 2024.

Alisema zaidi ya watoto milioni 20 wanakosa chanjo za kawaida, kwamba homa za msimu au dengue, na magonjwa mengine yanaongezeka kutokana na kuongezeka kwa joto duniani, na kwamba milipuko ya kipindupindu imetokea katika nchi zaidi ya 20 mwaka huu pekee. Aliongeza ushahidi unaonyesha kuwa “afya imejeruhiwa na vita”.

“Mamilioni ya watu nchini Sudan na Gaza wako katika hatari ya kufa, sio tu kutokana na risasi na mabomu, lakini kutokana na majeraha yasiyotibiwa na magonjwa”, alisema. “Mashambulizi yasiyo ya kawaida dhidi ya vituo vinavyotoa huduma za afya huenda zaidi ya kitu chochote ambacho nimeshuhudia katika wakati wangu kama katibu mkuu”.

Forum

XS
SM
MD
LG