Makubaliano mapya na Rwanda ni tofauti na mpango ulokwama wa serikali, wa kuwaondoa kwa lazima karibu waomba hifadhi wote kwenda katika nchi hiyo ya Afrika ya mashariki, ambayo mwaka jana mahakama kuu iliamuwa inakwenda kinyume cha sheria.
Badala yake inafanana na sera iliyoko ya serikali , ambayo waomba hifadhi wanapewa msaada wa kifedha kuondoka Uingereza na kwende kwenye nchi zao, lakini chini ya sheria mpya watapewa pesa endapo watakubali kuishi Rwanda.
Kevin Hollinrake, waziri mdogo wa biashara amesema siku ya Jumatano sera mpya itatumia vizuri fedha za umma kwa kuwa ni rahisi kuliko kuwatunza watu wakiwa Uingereza ambako wamenyimwa hifadhi, lakini bado hawajaondolewa.
Kuna maelfu ya waomba hifadhi ambao maombi yao yamekataliwa, lakini hawawezi kuondolewa kwa sababu serikali hairuhusiwi kuwarudisha watu katika nchi iliyokumbwa na vita au yenye rekodi mbaya ya haki za binaadamu.
Forum