Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:31

Wananchi wa Angola waanza kuondoka Namibia


Ramani ya Kusini mwa Afrika
Ramani ya Kusini mwa Afrika

Maafisa nchini Namibia wanasema maelfu ya wananchi wa Angola ambao waliingia nchini humo mwaka mmoja uliopita kuepuka nchini kwao, wamerejea baada ya mvua kuanza kunyesha.

Maafisa mwezi huu walisema takriban watoto wachanga 18 wa Angola, ambao wazazi wao walikimbia njaa, walifariki nchini Namibia kutokana na utapiamlo.

Kaimu Mkurugenzi wa Afya katika mkoa wa Omusati kaskazini mwa Namibia, Dr. Francina Ananias, alisema wahamiaji wengi wa Angola waliwasili nchini humo katika hali ambayo ni mbaya sana, na kupelekea vifo kadhaa vya watoto wachanga, ambao walifuata na mama zao ambao walikuwa wakitafuta chakula na maji.

“Tuliwafanyia tathmini na kubaini kwamba walikuwa na utapiamlo. Kwahiyo, tumekuwa tukiwapa lishe ambayo tulikuwa nayo ili waweze kurejea katika hali nzuri ya kawaida, lakini bahati mbaya, baadhi yao walifariki,” alisema Ananias.

Gavana wa mkoa wa Omusati, Erginus Endjala, ambaye alisimamia usalama wa wahamiaji kurejea Angola, alisema mvua za karibuni zilimshawishi kurejea nyumba ili kushughulikia shamba lake.

“Kwa muda wa miaka mitano iliyopita, hatukupata mvua za kutosha. Ina maana mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha ukame mbaya sana kwa eneo hilo la Angola, ambalo hivi sasa ni sehemu za kusini mwa Angola. Walipofika hapa uliweza kuona ukiangalia miili yao kwamba walikuwa na utapiamlo na kwa hakika, matokeo yake, baadhi ya watoto hao hawakuweza kunusurika kutokana na ukosefu wa chakula na pia mama zao hawakuwa na mazira ya kutosha kuwanyonyeshaz. Ndiyo sababu nadhani rekodi ya vifo vya watoto wachanga ilikuwa juu mno,” anasema Endjala.

Mwandishi wa habari wa eneo, Maria Davids alizungumza na baadhi ya wahamiaji ambao walikabidhiwa na serikali ya Namibia kwa Angola na kusema “walikuwa na hamu ya kurejea nyumbani, wakisema wako tayari kuanza tena maisha na kuungana tena naz familia zao.”

Nchini Namibia na Angola, matukio ya njaa, kote maeneo ya vijijini na mijini, yanaongezeka. Janga la Covid 19, ukame na mwenendo wa mabadiliko ya hali ya hewa yanabadili mafanikio yaliyopatikana katika misingi ya nchi zote kutimiza malengo ya maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG