Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 03:15

Wanajihadi wakishambulia kituo cha mafunzo ya kijeshi Mali na kuuwa watu zaidi ya 70


mkuu wa jeshi la Mali Oumar Diarra (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari huko Bamako Septemba 17, 2024
mkuu wa jeshi la Mali Oumar Diarra (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari huko Bamako Septemba 17, 2024

Shambulizi na wana jihadi katika mji mkuu wa Mali lililenga kituo cha mafunzo ya kijeshi na uwanja wa ndege ambapo watu zaidi ya 70 waliuawa na 200 kujeruhiwa, ikiwa ni moja ya idadi kubwa sana ya vifo kwa majeshi ya usalama katika miaka ya karibuni.

Chanzo cha usalama kikiongea katika misingi ya kutotajwa jina imeliambia shirika la habari la AFP kuwa watu 77 wameuawa na 255 wamejeruhiwa katika shambulizi la Jumanne mjini Bamako. Waraka wa siri wa serikali umeweka idadi ya vifo ni takriban 100 na kuwataja waathirika 81.

Toleo la gazeti la Le Soir limeripoti kwamba mazishi ya takriban wanafunzi wa kijeshi 50 huenda yakafanyika leo. Jumuiya ya Afrika Magharibi jana imelaani vikali mashambulizi ya Bamako ambako wenyeji wameelezea wasi wasi wao na kuhoji kuhusu shambulizi hilo.

Operesheni hiyo ilikuwa ya kwanza ya aina yake kwa miaka kadhaa na lilikuwa pigo kubwa kwa utawala wa kijeshi, watalaam wanasema.

Mji mkuu wa Mali kwa kawaida huwa haukumbwi na mashambulizi ambayo yanatokea kila siku katika baadhi ya sehemu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Siraha zinazodaiwa kukamatwa na jeshi huko Bamako
Siraha zinazodaiwa kukamatwa na jeshi huko Bamako

Maswali kuhusu jinsi wanajihadi walivyofanya shambulizi na kiwango cha uharibifu bado kimebaki.

Seydou Keita, dereva anasema hakuna udhibiti kwa watu wanaoingia mji mkuu kutokea kaskazini ambako waasi wanadhibiti eneo kubwa.

“Leo soko la Garbal huko Faladie mjini Bamako, ni tatizo. Nadhani walitumia mabasi makubwa kuingia Garbal, halafu na kujiingiza kwa raia kupitia Garbal. Tufanye msako huko Garbal, tutawapata baadhi ya washukiwa,” alisema.

Jama’at Nusrat al-Islam wal Muslimeen – kundi lenye msimamo mkali limedai kuhusika na shambulizi – picha zilizoonyeshwa ziliwaonyesha wapiganaji wakitembea wakizunguka na kufaytua risasi kiholela kwenye madirisha ya eneo la uwanja wa ndege ambalo hutumiwa na rais.

Kanda moja ya video ilimuonyesha mpiganaji akiwasha moto sehemu ya ndege.

Picha ya video ikionyesha moshi ukifuka angani katika mji wa Bamako
Picha ya video ikionyesha moshi ukifuka angani katika mji wa Bamako

Mamlaka haijasema chochote kama ndege ilikuwa ni ya mkuu wa utawala wa kijeshi Kanali Assimi Goita ndiyo ililengwa.

Miongoni mwa wasiojulikana ni idadi ya waliopoteza maisha, huku maafisa wakiwa bado hawajatoa idadi kamili ya vifo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jenerali Oumar Diarra, mkuu wa jeshi la Mali alisema, “Magaidi ambao waliingia katika shule ya kijeshi. Tunafanyakazi kuwakamata washirika na kuidhibiti hali.”

“Hii ni kazi yetu na sisi ni watalaamu. Nawaomba watu kutupatia habari. Nadhani uungaji mkono kutoka kwa umma umekuwa mkubwa, unaturuhusu kuwapata washukiwa hapa na pale, na uchunguziunaendelea. Magaidi wote hawana nguvu hapa,” aliongeza mkuu huyo wa jeshi la Mali.

Picha ya video iiliyochukuliwa na AFPTV ikionyesha Nguo na buti huko Bamako
Picha ya video iiliyochukuliwa na AFPTV ikionyesha Nguo na buti huko Bamako

Soumaila Tembely, mmiliki wa mgahawa anashangazwa kama kulikuwa na kiwango za uzembe kwa upande wa mamlaka.

“Kwa maoni yangu, kuna kiwango cha uzembe kwa upande wa mamlaka. Hali ya jshi la nchi wakati wote kuwa katika hali ya ulinzi. Tuseme hakuna kitu kipya. Hali imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu,” alisema.

Kulenga kambi za jeshi na uwanja wa ndege wa kijeshi, kundi la Jama’at Nusrat al-Islam wal Muslimeen limenonyesha nguvu yake siku ya Jumanne katika mji ambao haukuwahi kushuhudia mashambulizi makubwa.

Pia umejionyesha wakati ambapo lengo lilikuwa kaskazini mwa Mali. Huko, jeshi na washirika wake wa Russia kutoka kundi la mamluki la Wagner na taasisi mpya ya ulinzi inayojulikana kama Africa Corps wanajaribu kuwapata wa Tuarge wanaotaka kujitenga “ushindi wa kushangaza”, huku mmoja wa viongozi akisema dazeni ya raia wa Russia wameuawa. Kundi la JNIM limesema limewaua raia wa Russia 50 na 10 wa Mali.

Mapema mwaka huu, kikosi cha kupambana na ugaidi cha Barkhane cha Ufaransa, tume ya Umoja wa Mataifa kwa Mali MINUSMA, na wanajeshi wa Ulaya walidhibiti tisho la kaskazini, Hasn Jakob Schindler, mkuu wa Mradi wa Kukabiliana na Ugaidi aliiambia AFP.

Tangu wakati huo, amesema Schindler, “jeshi la Mali halijafanya kazi nzuri, Africa Corps wametenda ukatili dhidi ya jamii ya wenyeji,” na JNIM imefaidika kwa kutangaza kupitia propaganda zao kwamba inawalinda raia wa Mali.

Shambulizi la Jumanne asubuhi ilikuwa mfano wa maeandeleo ya kusonga mbele kuelekea kusini yaliyofanywa na wana Jihadi, ambao walielezea lengo lao ni kufika katika Ghuba ya Guinea kwa kushambulia mataifa ya pwani.

Mali, kama majirani zake na washirika Niger na Burkina Faso, wanaonepana kushindwa kusitisha mwenendo ulivyo.

Nchi za Magharibi, hivi sasa zinaonekana kama adui, hawana njia ya kukusanya habari za kipelelezi au kuchukua hatua.

Schindler anasema njia pekee ni kusitisha kusonga mbele kuelekea kusini kwa kufanya kazi na nchi za pwani, na kufikiria pengine kufanya kazi na washirika wa kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG