Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 06:01

Mali imesema mji mkuu Bamako ulidhibitiwa baada ya shambulio la waasi


Ramani ya Mali na nchi zilizo jirani nae.
Ramani ya Mali na nchi zilizo jirani nae.

Serikali ya kijeshi imesema baadhi ya maeneo nyeti ya mji mkuu yalishambuliwa ikiwemo shule ya mafunzo ya kijeshi.

Mali ilisema Jumanne kuwa mji mkuu Bamako ulikuwa umedhibitiwa baada ya waasi kushambulia shule ya mafunzo ya kijeshi na maeneo mengine majira ya alfajiri, wakifyatua risasi ambazo zilisikika kote mjini humo.

Mapema asubuhi ya leo, kundi la magaidi lilijaribu kuingia katika shule ya kijeshi ya Faladie. Operesheni za kuwasaka kwa sasa zinaendelea, jeshi limesema katika taarifa. Limetoa wito kwa wakazi kukaa mbali na eneo hilo na kusubiri mawasiliano rasmi.

Serikali ya kijeshi imesema baadhi ya maeneo nyeti ya mji mkuu yalishambuliwa ikiwemo shule ya mafunzo ya kijeshi. Ilisema jeshi limewarudisha nyuma magaidi waliohusika na shambulio hilo na liliwasihi raia kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Shule ya mafunzo ya kijeshi iko Faladie, wilaya iliyopo kusini mashariki mwa Bamako, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa. Shirika la habari la Reuters lilisikia milio ya risasi katika kitongoji cha Banankabougou karibu na Faladie kabla ya jua kuchomoza. Watu waliokuwa wakielekea msikitini kwa ajili ya sala ya alfajiri walirudi majumbani mwao wakati milio ya risasi ikisikika.

Forum

XS
SM
MD
LG