Mali ilikuwa tayari imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya waasi ndani na karibu na Tinzaouaten muda mfupi baada ya wapiganaji wa Tuareg na wapiganaji wenye msimamo mkali kuwauwa wanajeshi wengi wa Mali na mamluki wa Wagner wa Russia karibu na mji huo mwezi Julai.
Mji huo, uliopo karibu na mpaka wa Algeria, ulishambuliwa tena na ndege zisizo na rubani Jumapili, msemaji wa muungano wa waasi wa CSP amesema.
Mashambulizi yalipiga nyumba ya raia, duka la dawa na maeneo mengine ya mji, Mohamed Elmaouloud Ramadane amesema kwa njia ya simu. Takriban watu 15 wamethibitishwa kufariki dunia wakiwemo watoto, na idadi ya vifo huenda ikaongezeka, aliongeza.
Jeshi la Mali halikujibu maombi ya kuthibitisha taarifa hizi. Mapigano karibu na Tinzaouaten mwishoni mwa Julai yanaweza kuwa kipigo kikubwa zaidi cha Wagner tangu ilipoingia miaka miwili iliyopita kusaidia wanaharakati wa Mali kupambana na makundi ya waasi.
Waasi wa Tuareg wamesema wameuwa takriban mamluki 84 wa Wagner na wanajeshi 47 wa Mali. Tawi tanzu la al Qaida limesema limewauwa mamluki 50 wa Wagner na wanajeshi 10 wa Mali.
Si Mali wala Wagner walioweka wazi idadi ya wanajeshi waliofariki dunia, ingawa Wagner imesema imepata hasara kubwa.
Forum