Hayo ni kulingana na nakala ya barua yao iliyokuwa imechapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Msemaji huyo alisema kuwa wanamgambo wa eneo la Kaskazini mwa Mali wamepokea taarifa “muhimu” za kufanya mashambulizi ya mwezi Julai.
Katika barua yao, nchi hizo zinazoongozwa na jeshi zimeliomba baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa “kuvichukulia hatua” vitendo vya Ukrainen kuzuia “vitendo vya ugandamizaji”.
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine hakuweza kutoa majibu ya haraka lakini Ukraine imekuwa mara kwa mara ikituhumu tawala hizo za kijeshi kwa madai yasiyokuwa na msingi na ya uongo.
Mali ilikata uhusiano wa kidomokrasia na Ukraine mwanzoni mwa mwezi huu, ikifuatiwa na jirani yake Niger siku chache baadaye, kuhusiana na maoni yaliyotolewa na msemaji wa Ukraine wa ujasusi wa kijeshi.
Forum