Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:59

Nchi ya Mali imeamuru balozi wa Sweden mjini Bamako aondoke


Mji wa bamako nchini Mali
Mji wa bamako nchini Mali

Mivutano ya kidiplomasia inasisitiza jiografia pana ya mabadiliko yanayotokea katika eneo hilo

Balozi wa Sweden mjini Bamako, Kristina Kuhnel, ameamriwa kuondoka katika taifa hilo la sahel huko Afrika Magharibi ndani ya saa 72, wizara ya mambo ya nje ya Mali imesema leo Ijumaa, kwa sababu ya kile ilichokiita taarifa ya “chuki” iliyotolewa na Waziri wa Sweden.

Mivutano ya kidiplomasia inasisitiza jiografia pana ya mabadiliko yanayotokea katika eneo hilo katika mataifa matatu yanayoongozwa na utawala wa kijeshi - Mali, Burkina Faso na Niger, yakijitenga na ushirika wa jadi wa Magharibi na kujiunga na Russia.

Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na biashara wa Sweden, Johan Forssell, alisema Jumatano kuwa serikali iliamua kusitisha misaada kwa Mali kutokana na uhusiano wake na Moscow.

“Huwezi kuunga mkono vita vya Russia visivyo halali vya uchokozi dhidi ya Ukraine na wakati huo huo kupokea mamilioni kadhaa ya fedha kila mwaka katika misaada ya maendeleo,” Forssell alisema, akijibu kwenye chapisho lililobandikwa katika mtandao wa X ambao ulisema Mali ilikata uhusiano na Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG