Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 19:35

Wanajeshi wa Ukraine wazima mashambulizi kadhaa ya Russia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (Ukrainian Presidential Press Office via AP)
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (Ukrainian Presidential Press Office via AP)

Wanajeshi wa Ukraine wamezima mashambulizi kadhaa ya Russia mashariki mwa nchi hiyo, shirika la kijasusi la Uingereza limesema Jumatatu.

Wakati huo huo Rais Volodymyr Zelenskyy alisema maelfu ya wanajeshi wa Russia wanajipanga kwa mashambulizi mapya.

Vikosi vya Russia pia vimekuwa vikishinikiza kupata udhibiti juu ya mji wa kusini wa bandari wa Mariupol kiunganishi kati ya maeneo yanayoshikiliwa na Russia upande wa magharibi na mashariki.

“ Kuna maelfu ya watu waliokufa , lakini licha ya hilo, Russia haijaacha mashambulizi yake,” Zelensky aliliambia bunge la Korea Kusini kwa njia ya video.

Shirika la habari la ROITA halijathibitisha uhakika wa makadirio yake.

Uvamizi wa Russia, mzozo mkubwa bara Ulaya tangu vita vya Balkans vya mwaka 1990, umesababisha vifo ambavyo vimezua ukosoaji mkubwa wa nchi za Magharibi na wasiwasi juu ya matarajio mapana ya Putin.

XS
SM
MD
LG