Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alionya Alhamis kwamba ripoti zaidi za kuaminika za ukatili wa Russia dhidi ya raia wa Ukraine zinatoka katika nchi hiyo iliyoharibiwa na vita na kuapa kwamba siku moja kwa namna fulani kutakuwa na uwajibikaji kwa Moscow.
Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani baada ya kukutana na NATO na washirika mawaziri wa mambo ya nje mjini Brussels alisema alichukizwa na kile serikali ya Russia inachokifanya.
Alielezea tukio moja la mashambulizi ya Russia kwenye kitongoji cha Bucha katika mji mkuu wa Kyiv ambapo miili 410 ya raia wa Ukraine imepatikana wengi wao wakiwa wamekufa mitaani kabla ya wanajeshi wa Russia kujiondoa na kuanzisha mashambulizi mapya kusini na mashariki mwa Ukraine.