Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 10:25

Ukraine inasema ikipata silaha itajilinda vilivyo dhidi ya Russia


Moshi mzito uliotanda juu ya mji wa Kyiv, Ukraine, kufuatia mabomu yaliyorushwa na wanajeshi wa Russia.
March 25, 2022. PICHA: AP
Moshi mzito uliotanda juu ya mji wa Kyiv, Ukraine, kufuatia mabomu yaliyorushwa na wanajeshi wa Russia. March 25, 2022. PICHA: AP

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amepuuza hatua ya baadhi ya nchi kusita kutekeleza maombi ya silaha kwa nchi hiyo kutokana na wasiwasi kwamba huenda zikajiingiza moja kwa moja katika mzozo na Russia.

Kuleba amesema kwamba kwa kuipatia Ukraine msaada huo, raia wa Ukraine watapigana wenyewe na hakuna mtu mwingine atatakiwa kufanya hivyo.

Alikuwa akizungumza mjini Brussels, akiwa na katibu mkuu wa muungano wa NATO Jens Stoltenberg, kabla ya kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa NATO.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ukraine amesema wana Imani kwamba njia bora zaidi ya kuisaidia Ukraine ni kuipatia msaada wa silaha ili kukabiliana na wanajeshi wa Russia walio Ukraine na kuhakikisha kwamba vita hivyo havisambai na kuingia nchi nyingine.

Stoltenberg amesema kwamba nchi wanachama wa NATO watashughulikia mahitaji ya Ukraine katika kujilinda. Amezitaka nchi za magharibi kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya Russia ikiwemo kuweka marufuku ya kununua mafuta ya Russia, kuzuia benki zote za Russia kupokea au kutuma pesa nje ya nchi na kufunga bandari zote kwa meli na bidhaa kutoka Russia.

XS
SM
MD
LG