Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:21

Biden amtaja Putin kuwa mhalifu wa kivita kufuatia picha za mauaji Ukraine


Ira Gavriluk akiwa amebeba paka wake, akipita karibu na miili ya watu waliouawa akiwemo mme wake, ndugu na mwanamme asiyejulikana nje ya nyumba yao, Bucha, nje ya mji wa Kyiv, Ukraine, April 4, 2022.
Picha: AP
Ira Gavriluk akiwa amebeba paka wake, akipita karibu na miili ya watu waliouawa akiwemo mme wake, ndugu na mwanamme asiyejulikana nje ya nyumba yao, Bucha, nje ya mji wa Kyiv, Ukraine, April 4, 2022. Picha: AP

Rais wa Marekani Joe Biden ametaka jopo maalum kuanzishwa kuchunguza na kufungua mashtaka kuhusiana na uhalifu wa kivita katika mji wa Bucha, nchini Ukraine.

Biden amesema kwamba anataka vikwazo zaidi dhidi ya Russia.

Amemtaja rais wa Russia Vladmir Putin kuwa mhalifu wa vita na kwamba mauaji hayo ni uhalifu wa vita.

Mara ya kwanza Biden alimtaja Putin kuwa mhalifu wa vita, Kremlin ilijibu kwa hasira sana.

Marekani na muungano wa NATO hawataki kuingia katika mgogoro wa moja kwa moja na Russia ambayo ina silaha za nuclear, na badala yake wametoa msaada wa silaha na pesa kwa Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Russia, huku wakiwekea Russia vikwazo vikali ambavyo vimeanza kuathiri uchumi wake.

Matamko ya Biden yanafuatia kutolewa picha za kutisha za miili ya watu walioua katika vita vya Ukraine kutokana na mashambulizi ya mjini Bucha.

Picha hizo zimetolewa baada ya wanajeshi wa Russia kuondoka sehemu hiyo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mkuu wa ofisi ya haki za kibinadamu wa umoja wa mataifa Michelle Bachelet, amesema kwamba kuna uwezekano kwamba kulitokea uhalifu wa kivita, kukiukwa kwa sheria ya kimataifa na haki za kibinadamu.

Maafisa wa Ukraine katika mji wa Bucha wamesema kwamba wamelazikika kuchimba makaburi ya pamoja ili kuzika miili kadhaa wa watu waliouawa na kuzuia miili hiyo kujazana barabarani.

Baadhi ya watu waliouawa walikuwa wamefungwa mikono.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine Lryna Venediktova amesema kwamba zaidi ya miili 410 imepatikana kufikia sasa.

Ofisi ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa imesema kwamba maafisa wako katika sehemu hiyo ya tukio kuthibitisha idadi ya watu waliouawa.

XS
SM
MD
LG