Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 11:42

Boris asema Putin amechafua sifa yake


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, kushoto, na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, akiwa Kyiv, Ukraine, Jumamosi, April 9, 2022. (Ukrainian Presidential Press Office via AP)
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, kushoto, na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, akiwa Kyiv, Ukraine, Jumamosi, April 9, 2022. (Ukrainian Presidential Press Office via AP)

Kugunduliwa kwa miili ya raia katika miji ya Ukraine “kutaendelea kuchafua” sifa ya Rais wa Russia Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema wakati wa ziara yake mjini Kyiv Jumamosi.

Kugunduliwa kwa miili ya raia katika miji ya Ukraine “kutaendelea kuchafua” sifa ya Rais wa Russia Vladimir Putin, Waziri wa Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema wakati wa ziara yake mjini Kyiv Jumamosi.

Kile ambacho Putin amekifanya katika maeneo kama Bucha na Irpin ni uhalifu wa kivita ambao utaendelea kuchafua hadhi yake na ya serikali yake,” Johnson alisema, akiwa pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Johnson alikuwa ni kiongozi wa Ulaya hivi karibuni kuzuru Kyiv mwishoni mwa wiki baada ya miili kugunduliwa katika miji kadhaa ambako majeshi ya Russia yaliondoka.

Ukraine 'yakabili hali mbaya'

Johnson aliipongeza Ukraine kwa “kuweka msimamo” na kukabiliana na uvamizi wa Russia huko Ukraine.

“Warussia waliaamini Ukraine ingeweza kuchukuliwa katika kipindi cha siku kadhaa na kwamba Kyiv itaangukia katika mikono ya majeshi yao,” alisema, akizungumzia habari za kijasusi za Magharibi.

“Walikuwa hawako sahihi,” alisema.

Wananchi wa Ukraine “wameonyesha ushujaa wa simba,” alisema.

“Dunia imegundua mashujaa wapya na mashujaa hao ni watu wa Ukraine,” Johnson alisema.

Baada ya mazungumzo na Zelenskyy, Johnson aliahidi Uingereza itaipa Ukraine magari ya kivita na mifumo ya makombora ya kuzuia mashambulizi ya Russia.

Zelenskyy alizitaka nchi za Magharibi kufuata mfano wa Uingereza wa kutoa misaada ya kijeshi kwa Ukraine na kuiwekea vikwazo Russia.

“Nchi nyingine za kidemokrasia za Magharibi zifuate mfano wa Uingereza,” Zelenskyy alisema baada ya mazungumzo na Johnson.

XS
SM
MD
LG